Wednesday, 28 January 2015

Andre Ayew aipeleka Ghana Robo fainali AFCON


CAIRO, Misri
MSHAMBULIAJI nyota  Andre Ayew aliipa Ushindi Muhimu Timu yake ya Ghana uliopa tikeki ya kucheza  Robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika katika kundi C, baada ya kuilaza South Afrika kwa mabao 2-1.

Vijana wa Kocha Avram Grant walikuwa wa kwanza kufunga Ubao wa mabao baada ya staika wake Mandla Masango kuweka kimiani bao la kwanza mnamo dakika ya 17, lililodumu kipindi cha kwanza.
Alikuwa  John Boye aliyebadilisha matokeo ndani ya dakika 17 baadae ushindi ulioupa Ghana nguvu ya kushambulia ngome ya Afrika Kusini.
Hata hivyo, Ayew alifunga ubao wa mabao kwenye dakika 83, na kuihakikishia Ghana kuingia raundi ya pili.
Ghana, ilimungiza nyota wake Wakaso Mubarak aliyechukua nafasi ya Emmanuel Agyemang-Badu, lakini bado ilikuwa moto wa kuotea mbali, ingawa wasiwasi ulienea kwa kutokosekana kwenye mchezo kwa nyota wa Afrika Kusini, Khuzwayo baada ya kusumbuliwa na  misuli nusu saa kabla ya mpira kuanza.

Wakati huo huo Senegali imejikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kupokea kipigo kilichovunja rekodi yao dhidi ya Algeria, kufuatia kuzabwa mabao 2-0. 
Senegal imesogea hadi nafasi ya tatu nyuma ya Algerians baada Ghana kuibuka na Ushindi dhidi ya Afrika Kusini.

Algeria ilikuwa bora katika dakika nane za kipindi cha pili baada ya staika Nabil Bentaleb kuzifumania nyavu za Senegal kabla ya
Riyad Mahrez kufunga bao la kwanza katika mchezo uliopigwa katika dimba la Mongomo.



Aidha Algeria, hawakuwa na madhara yeyote katika dakika 20 za mwanzo wa mchezo baada ya kuandamwa na Senegal.  

IMEANDALIWA NA GILBERT MASSAWE KWA MSAADA WA MASHIIRIKA YA HABARI

No comments:

Post a Comment