na salma juma
Mechi
za kwanza za raundi ya pili ya mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu
kwa wanawake-Tanzania (Taifa Cup Wanawake) zinachezwa wikiendi hii
(Januari 17 mwaka huu) kwenye miji minane tofauti nchini.
Timu
tisa zilizofuzu kutoka raundi ya kwanza baada ya mechi za nyumbani na
ugenini akiwemo mshindwa (best loser) zitaungana na Ilala, Kinondoni na
Temeke kucheza raundi ya pili. Mechi za marudiano za raundi hiyo
zitachezwa Januari 21 mwaka huu.
Hatua ya robo fainali
itakayochezwa Januari 26 na 27 mwaka huu pamoja na nusu fainali na
fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Proin Promotions itafanyikia
jijini Dar es Salaam. chanzo. bbc swahili.com
No comments:
Post a Comment