Wanafunzi wa Chuo Cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) wakisaidiana na mwalimu wao wa somo la PUBLIC RELATION kuzoa takataka katika soko la mbauda jijini arusha.picha na.SUZANE CHEDDY |
hayo yamesemwa na mwenyekiti wa mtaa wa kirika A Bw.PROSPER MOLLEL wakati akiongea na kuwashukuru wanafunzi wa Chuo Cha Uandishi Wa Habari Na Utangazaji Arusha ofisini kwake baada ya kujitolea kufanya usafi katika soko la mbauda.
pamoja na kufanya usafi kila mara pia kuna ratiba ya kufanya usafi kila mwezi ambapo usafi huo hujumuisha jamii kwa ujumla na kusema usafi njia moja wapo ya kuzuia milipuko ya magonjwa na kuweka picha nzuri kwa jamii inayotuzunguka.
" usafi ukiwepo wa kutosha kunaepusha ule mlipuko wa magonjwa na kuingiza serikali gharama ya kutoa matibabu."Amesema Bw.PROSPER MOLLEL Mwenyekiti wa mtaa.
mwenyekiti ameushkuru uongozi wa chou kwa kujitolea na kuwapumnzisha wafanyakazi wao.pia amesema kuna uhaba wa wafanyakazi hivyo kupelekea wakati mwingine usafi haufanyiki kwa usahihi.hivyo ni vyema waatu kujitokeza kushiriki katika kuweka eneo hilo na jiji kwa ujumla katika hali ya usafi.
CHANZO:SUZANE CHEDDY
No comments:
Post a Comment