Na Gilbert Massawe, Arusha
AFISA wa Afya katika kata ya
Sombetini jijini Arusha, Beatha Gtaguo, amekipongeza chuo Cha Uandishi
wa habari na Utangazaji Arusha, kufuatia
kujitolea kufanya Usafi katika soko la mbauda kama mchango wao kwa jamii.
Akizungumza na website ya chuo Beatha Gitaguo alisema
kuwa wamefurahishwa na jambo hilo kwani
ni ushirikiano mzuri kati ya chuo na jamii inayowazunguka na kufanya hivyo ni
kuwaelimisha wananchi wengine kujitolea
katika kazi za jamii.
Hata hivyo, Wanafunzi wa Chuo cha
Uandishi wa habari wamejitolea kufanya usafi katika soko hilo kama mojawapo
ya shughuli za kijamii ili kuonyesha mfano mzuri kwa jamii inayowazunguka.
“Tumeshukuru kwa ujio wenu na kutuunga mkono
katika swala la usafi na wanajamii wamejiuliza maswali kutokana na kile
mlichokifanya eneo hili,” alisema Beatha
Alisema mojawapo mwa changamoto inayoikabili
soko hilo ni Uhaba wa wafanyakazi wa kufagia, ambapo wapo wafanyakazi watatu wanaosafisha
eneo hilo na miundo mbinu ya soko hilo haijakaa sawa hivyo huwapa wafagiaji
tabu wakati wa ufagiaji.
No comments:
Post a Comment