Na ; Yusuph Mbata
Arusha
Chuo cha
uandishi wa habari na utangazaji Arusha{AJTC}, kimesifiwa na uongozi wa soko la
Mbauda, kufuatia usafi uliofanywa na wanafunzi wa chuo hicho siku ya juma nne asubuhi.
Akitoa
shukrani hizo wakati akizungumza na waandisi wa habari, afisa masoko wa kata ya
Sombetini Bi. Beatha Gitagno. Amesema ni kitendo cha aina yake kilichofnywa na
wanafunzi hao, na nivyema kuigwa na hata jamii nzima.
‘’Kwakweli tumefurahishwa sana kitendo hiki kilihofanywa na
wanachuo hawa, sababu ni wanafunzi
wachache sana wanaweza kujitoa kufanya kazi za kijamii’’ alisema bi. Beatha
Wanafunzi kutoka chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la mbauda jijini Arusha (Picha na Yusuph Mbata , ruaha class) |
Hata hivyo baadhi ya wafanya biashara katika soko hilo,
wametoa wito pia kwa vyuo vingine kuiga kile kilichofanywa na wanafunzi hao.
Kwakuwa itawajenga kiakili, kimwili hata kujenga ushirikiano na jamii.
Mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho,aliyejitambulisha kwa jina
la Mbaraka Yahaya amesema hiyo kwao ni
moja ya masomo. Hivyo ni wajibu wao kufanya hivyo na nilazima wajifunze kwa
nadharia na vitendo pia.
‘’Sisi hii kwetu ni moja ya masomo, na ili kufikia malengo
yetu. Ni lazma tujifunze kwa vitendo zaidi. Kuna somo linaitwa Public Relations
,kutoka kwenye kipengele cha PR campaign ambapo ilitulazimu kufanya kazi za
kijamii.’’ Mbaraka alisema
Kwa upande wa Mkufunzi wa chuo hicho, ambae pia ni mwalimu wa
somo hilo Madam Velediana. Alitoa shukrani zake kwa uongozi wa soko hilo, kwani
walipokelewa kwa ukarimu tangu siku ya kwanza. Na kuonyeshwa ushirikiano
wakutosha kutoka kwa viongozi hao.
No comments:
Post a Comment