Wednesday, 11 February 2015

UONGOZI WA SOKO LA MBAUDA UMEWASHUKURU WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI NA UTANGAZAJI KWA KUJITOLEA KUFANYA USAFI SOKONI HAPO.



Na ; Calorine Marwa.
Arusha
 
Wanafunzi wa madarasa ya Ruaha na Tarangire katika chuo cha uandishi wa habari na uatanagazaji Arusha wamefanya usafi katika soko la Mbauda ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao ya vitendo .

Baadhi ya wanafunzi hao wamesema kuwa wamefanya kazi hiyo kwa lengo la kujenga uhusiano mzuri na jamii pamoja na kutangaza jina la chuo na kijiweka katika nafasi nzuri 
Wanafunzi kutoka chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la mbauda jijini Arusha. (Picha na Calorine Marwa , ruaha media)
.Naye kwa upande wake Afisa wa afya wa kata ya Sombetini Bi. Betha Kitagoamewashukuru wanafunzi hao kwa kuwaunga mkono katika swala la usafi na kuahidi kuwaelimisha waliopo nyuma yao kwa kuendeleza usafi katika eneo hilo .

Bi . Gitago amesema kuwa wanakabiliwa na tatizo la wafagiaji wa soko hilokwani wapo watatu tu jambo ambalo linarudisha nyuma suala nzima la uasafi  katika soko hilo .

Aidha mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo Bw Hassan Athuman amesema amefurahishawa na zoezi hilo na kuwapongeza wanafunzi hao kwa kujitolea kufanya usafi n a kuwaomba waendeleena umoja huu ili kujenga uhusiano mzuri na jamii 

No comments:

Post a Comment