Wednesday, 11 February 2015

UONGOZI WA SOKO LA MBAUDA UMEWASHUKURU WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI NA UTANGAZAJI KWA KUJITOLEA KUFANYA USAFI SOKONI HAPO.

Na Pendo Mbasee
Arusha
 
Mwenyekiti wa kata ya Sombetini bw.Prosper mollel ametoa shukrani kwa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha kwa kufanya usafi katika soko la Mbauda jijini Arusha.
 

  Wanafunzi kutoka chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la mbauda jijini Arusha.  (Picha na Pendo  Mbasee) 
Ametoa shukrani hizo leo asubuhi alipokuwa akizungumza na wanafunzi hao mara baada ya zoezi hilo kumalizika ambapo amesema kuwa wamesaidia sana katika    kuweka mazingira ya soko hilo kuwa saf.i


Naye bi. Afya wa kata hiyo Beatha Gitaguo amewashukuru wanafunzi hao kwa kuwaunga mkono katika suala la usafi na kusema kuwa itakuwa fundisho kwa wanafunzi na watu wengine kufanya kitendo kama hicho katika maeneo mbalimbali yanayowazunguka.



Amesema soko hilo limekuwa chafu kwa muda mrefu licha ya kuwa wawakilishi kutoka halmashauri ya jiji wamekuwa wakilisafisha lakini bado hali ya uchafu inaongezeka kutokana na wawakilishi hao kuwa wachache na  kukosa ushirikiano kutoka kwa wananchi
Kwa upande wa wanafunzi hao wamesema suala la kujitoa kufanya shughuli za kijamii kama kufanya usafi sehemu mbalimbali,kutembelea vituo vya watoto yatima hata wagonjwa,ni wajibu wa kila mtu na siyo wahusika pekee.
Wamesema lengo lao la kufanya hivyo ni kujenga na kudumisha uhusiano baina yao na jamii inayowazunguka kwani wao ni sehemu ya jamii na jamii ni wao hivyo ni jukumu lao kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment