Arusha
Jamii imeaswa
kuwa mfano wa kujitolea kufanya usafi katika maeneo mbali mbali yanayo
wazunguka katika makazi yao yakiwamo hospitali,sokoni na vituo vya mabasi
Hayo
yamesemwa na Bi Atha Beatha ambaye ni
afisa ugani wa Afya wa kata ya sombetini mjini Arusha leo wakati
akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa habari na Utangazaji Arusha
(AJTC) mara tuu baada yakumaliza zoezi lakufanya usafi katika soko la Mbauda.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la Mbauda jijini Arusha ( Picha na Alexander Magige, ruaha class) |
Bi, Beatha amesema kuwa ni vizuri jamii
ikajifunza kufanya usafi katika sehemu mbalimbali zinazowazunguka ili kujikinga
na magonjwa nyemelezi yasababishwayo na uchafu yakiwepo homa za
matumbo,kipindupindu, nahata malaria.
Aidha Bi
Beatha amezitaka taasisi mbalimbali kuiga mfano wakufanya kazi za kijamii kama walivyofanya wanafunzi wa Chuo cha
Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha kwani zipo changamoto nyingi
zinazowakabili makundi tofauti ndani ya jamii.
Hatahivyo
baadhi ya wafanyabiashara wa soko la mbauda wamekipongeza chuo hicho kwa kazi
yao nzuri na kuahidi kuendeleza kuweka soko hilo katika hali ya usafi na siyo
hadi kusubiri taasisi mbalimbali zinazojitolea.
Nae
mfanyabiashara mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Juma Selemani
maesema kuwa
zipo changamoto mbalimbali zinazowakabili katika kuweka mazingira ya soko hilo
katika hali ya usafi ikiwemo kutokuwepo kwa mifereji yakusafirisha maji taka
pamoja na wamiliki wa majumba yaliyopo sokoni hapo kutiririsha maji machafu
sokoni hapo.
Chuo cha
Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha kimekuwa na desturi yakufanya kazi za
kijamii sehemu mbalimbali zikiwepo
kufanya usafi katika maeneo tofautitofauti hapa mjini Arusha, Kutoa
misaada mbalimbali kwa wasiojiweza wakiwepo watoto yatima.
No comments:
Post a Comment