Na Zainabu Thabiti
Arusha
Wakazi wa
Mbauda wamekipongeza chuo Cha Uandishi
wa habari na Utangazaji Arusha kwa
kujitolea kufanya usafi katika soko la mbauda kama mchango wao kwa jamii.
Akizungumza
na wanafunzi hao pamoja na waandishi wa
habari waliofika sokoni hapo Afisa afya
wa kata ya Sombetini Beatha Gitaguo alisema kuwa wamefurahishwa na jambo
hilo kwani ni ushirikiano mzuri kati ya
chuo na jamii inayowazunguka na kuwa kwa kufanya hivyo ni kuwaelimisha walioko nyuma yao .
“Tumeshukuru
sana kwa ujio wenu wakuamua kutuunga
mkono katika swala la usafi na hivi mlivyofanya hata wanajamii wamejiuliza
maswali kama nyinyi msiyohusika na soko
hili mmeamua kufanya usafi je wao si zaidi katika kufanya hivyo” alihoji Beatha
Hata hivyo
alisema kuwa katika soko hilo linakabiliwa na
uhaba wa wafanyakazi wa kufagia
ambapo alisema wapo watatu kwa eneo lote na kuongeza kuwa miundo mbinu
ya soko hilo haijakaa sawa hivyo huwapa wafagiaji tabu wakati wakufagia.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la Mbauda jijini Arusha (Picha na Zainabu Thabiti , ruaha class) |
Naye mkufunzi wa chuo hicho Verediana Akonaye alisema lengo lao kufanya hivyo ni
ili kujenga mahusiano mazuri na jamii na kama waandishi wa habari na maafisa
uhusiano watarajiwa ni lazima
kuchangamana katika shughuli za kijamii.
Aliongeza
kuwa chuo hicho pia kinaandaa maafisa mahusiano hivyo
kazi za kijamii ni moja ya aina za kampeni ya kuhamasisha kampeni za kampuni flani.
Kwa upande
wake mmoja wa wafanya biashara wa soko
hilo Hassani Athumani alisema kuwa wao
kama wafanya biashara wamefurahishwa na jambo hilo kwa kuwa usafi ni nyenzo
muhimu kwa maisha ya binadamu ambapo aliongeza
kuwa kutokana na uchache wa wafagiaji wa soko hilo wamekuwa wakizidiwa na
wakati mwingine kushindwa kufanya vizuri.
Naye
mwanafunzi Salma Juma wa darasa la Ruaha amesema amefurahishwa na mapokezi
waliyoyapa toka sokoni hapo na kudai kuwa kujitolea kufanya usafi sokoni hapo
no moja ya masomo yao wanayojifunza
chuoni hapo
MWISHO.
No comments:
Post a Comment