.
Na ; Angela
Raphael , Ruaha Class.
Arusha
Wanafunzi wa
madarasa ya Ruaha na Tarangire katika chuo cha uandishi wa habari na
uatanagazaji Arusha wamefanya usafi katika soko la Mbauda ikiwa ni sehemu ya
mafunzo yao ya vitendo .
Katika picha ni wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la Mbauda kwa lengo la kutengeneza uhusiano mzuri na jamii (Angela Raphael , Ruaha Class.) |
Baadhi ya
wanafunzi hao wamesema kuwa wamefanya kazi hiyo kwa lengo la kujenga uhusiano
mzuri na jamii pamoja na kutangaza jina la chuo na kijiweka katika nafasi nzuri
.
Naye kwa
upande wake Afisa wa afya wa kata ya Sombetini Bi. Betha Kitagoamewashukuru
wanafunzi hao kwa kuwaunga mkono katika swala la usafi na kuahidi kuwaelimisha
waliopo nyuma yao kwa kuendeleza usafi katika eneo hilo .
Bi . Gitago
amesema kuwa wanakabiliwa na tatizo la wafagiaji wa soko hilokwani wapo watatu
tu jambo ambalo linarudisha nyuma suala nzima la uasafi katika soko hilo .
Aidha mmoja
wa wafanyabiashara katika soko hilo Bw Hassan Athuman amesema amefurahishawa na
zoezi hilo na kuwapongeza wanafunzi hao kwa kujitolea kufanya usafi n a
kuwaomba waendeleena umoja huu ili kujenga uhusiano mzuri na jamii
No comments:
Post a Comment