Wednesday, 11 February 2015

WANAFUNZI KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI AJTC KATIKA SOKO LA MBAUDA JIJINI ARUSHA WAKIFANYA USAFIM

RUAHA CLASS
PICHA NA ;HAPPYNESS ERNEST.

Mmoja wa wanafunzi HAPPYNESS ERNEST akiwa na wenzake wakifanya usafi katika soko la mbauda jijini arusha hapo jana.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la ruaha katika mkakati wa kufanya usafi mbauda sokoni kulia akiwa ni Pendo mbasse,pembeni yake ni Ester Danford akifatiwa na Agness kinisa,Dula wella,pamoja nae Elizabeth betha.

Mwenyekiti wa mtaa wa kirika A Bwana PROSPER MOLLEL akitoa shukurani zake kwa wanafunzi wa AJTC  na uongozi wake baada yakumalizika kwa usafi mbauda sokoni hapo jana







Wanafunzi wa madarasa ya ruaha  na tarangire wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha wamefanya  usafi katika soko la mbauda lililopo jijini arusha hapo jana ikiwa ni moja ya somo lao kw a vitendo.


Wanafunzi  hao wa chuo hicho wameeleza kuwa  dhumuni kubwa  lililowapelekea  kufanya usafi katika soko hilo  ni kwa ajili ya kujenga uhusiano mzuri baina yao na jamii kwa ujumla.

Akizungumza na RUAHA CLASS BLOG Afisa wa kata ya sombetini Bi BETHA GITAGNO alisema  amefurahishwa na kitendo  kilicho fanywa na wanafunzi wa AJTC na uongozi wake  kwamba wamefanya jambo la pekee na la kuigwa  na jamii au wanafunzi wengne.

''kwa kweli mmefanya jambo la pekee sana nalakuigwa na mmenifuraisha sana  kwa jinsi mlivyo jitolea kusaidia jamii yetu ''Aliseama BETHA GITAGNO.

Hata hivyo  mwenyekiti wa mtaa wa kiriaA Bwana PROSPER MOLLEL aliitimisha kwa kutoa shukrani  zake za dhati kwa wanafunzi wa AJTC na uongozi wake  kwa umoja na ushirikiano  walionesha katika kufanya usafi  katika soko hilo.
CHANZO;HAPPY ERNEST.

No comments:

Post a Comment