Wednesday, 11 February 2015

CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA {AJTC} CHAJIZOLEA SIFA KUTOKA UONGOZI WA SOKO LA MBAUDA.


Na Mbaraka Yahaya
Arusha
Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha{AJTC}, kimesifiwa na uongozi wa soko la Mbauda, kufuatia usafi uliofanywa na wanafunzi wa chuo hicho siku ya juma nne asubuhi.

Akitoa shukrani hizo wakati akizungumza na waandisi wa habari, afisa masoko wa kata ya Sombetini Bi. Beatha Gitagno. Amesema ni kitendo cha aina yake kilichofnywa na wanafunzi hao, na nivyema kuigwa na hata jamii nzima.

‘’Kwakweli tumefurahishwa sana kitendo hiki kilihofanywa na wanachuo hawa, sababu  ni wanafunzi wachache sana wanaweza kujitoa kufanya kazi za kijamii’’ alisema bi. Beatha
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la Mbauda jijini Arusha ( Picha na Mbaraka Yahaya , ruaha class)
 
Hata hivyo baadhi ya wafanya biashara katika soko hilo, wametoa wito pia kwa vyuo vingine kuiga kile kilichofanywa na wanafunzi hao. Kwakuwa itawajenga kiakili, kimwili hata kujenga ushirikiano na jamii.

Mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho,aliyejitambulisha kwa jina la Mbaraka Yahaya  amesema hiyo kwao ni moja ya masomo. Hivyo ni wajibu wao kufanya hivyo na nilazima wajifunze kwa nadharia na  vitendo pia.

‘’Sisi hii kwetu ni moja ya masomo, na ili kufikia malengo yetu. Ni lazma tujifunze kwa vitendo zaidi. Kuna somo linaitwa Public Relations ,kutoka kwenye kipengele cha PR campaign ambapo ilitulazimu kufanya kazi za kijamii.’’ Mbaraka alisema

Kwa upande wa Mkufunzi wa chuo hicho, ambae pia ni mwalimu wa somo hilo Madam Velediana. Alitoa shukrani zake kwa uongozi wa soko hilo, kwani walipokelewa kwa ukarimu tangu siku ya kwanza. Na kuonyeshwa ushirikiano wakutosha kutoka kwa viongozi hao.

JAMII IMEASWA KUZINGATIA USAFI.

Na Alexander Magige
Arusha



Jamii imeaswa kuwa mfano wa kujitolea kufanya usafi katika maeneo mbali mbali yanayo wazunguka katika makazi yao yakiwamo hospitali,sokoni na vituo vya mabasi

Hayo yamesemwa na Bi Atha Beatha ambaye ni  afisa ugani wa Afya wa kata ya sombetini mjini Arusha leo wakati akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa habari na Utangazaji Arusha (AJTC) mara tuu baada yakumaliza zoezi lakufanya usafi katika soko la Mbauda.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la Mbauda jijini Arusha ( Picha na Alexander Magige, ruaha class)
 Bi, Beatha amesema kuwa ni vizuri jamii ikajifunza kufanya usafi katika sehemu mbalimbali zinazowazunguka ili kujikinga na magonjwa nyemelezi yasababishwayo na uchafu yakiwepo homa za matumbo,kipindupindu, nahata malaria.

Aidha Bi Beatha amezitaka taasisi mbalimbali kuiga mfano wakufanya kazi za kijamii   kama walivyofanya wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha kwani zipo changamoto nyingi zinazowakabili makundi tofauti ndani ya jamii.

Hatahivyo baadhi ya wafanyabiashara wa soko la mbauda wamekipongeza chuo hicho kwa kazi yao nzuri na kuahidi kuendeleza kuweka soko hilo katika hali ya usafi na siyo hadi kusubiri taasisi mbalimbali zinazojitolea.

Nae mfanyabiashara mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Juma Selemani
 maesema kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazowakabili katika kuweka mazingira ya soko hilo katika hali ya usafi ikiwemo kutokuwepo kwa mifereji yakusafirisha maji taka pamoja na wamiliki wa majumba yaliyopo sokoni hapo kutiririsha maji machafu sokoni hapo.

Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha kimekuwa na desturi yakufanya kazi za kijamii sehemu mbalimbali zikiwepo  kufanya usafi katika maeneo tofautitofauti hapa mjini Arusha, Kutoa misaada mbalimbali kwa wasiojiweza wakiwepo watoto yatima.

UONGOZI WA SOKO LA MBAUDA UMEWASHUKURU WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI NA UTANGAZAJI KWA KUJITOLEA KUFANYA USAFI SOKONI HAPO.

Na Pendo Mbasee
Arusha
 
Mwenyekiti wa kata ya Sombetini bw.Prosper mollel ametoa shukrani kwa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha kwa kufanya usafi katika soko la Mbauda jijini Arusha.
 

  Wanafunzi kutoka chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la mbauda jijini Arusha.  (Picha na Pendo  Mbasee) 
Ametoa shukrani hizo leo asubuhi alipokuwa akizungumza na wanafunzi hao mara baada ya zoezi hilo kumalizika ambapo amesema kuwa wamesaidia sana katika    kuweka mazingira ya soko hilo kuwa saf.i


Naye bi. Afya wa kata hiyo Beatha Gitaguo amewashukuru wanafunzi hao kwa kuwaunga mkono katika suala la usafi na kusema kuwa itakuwa fundisho kwa wanafunzi na watu wengine kufanya kitendo kama hicho katika maeneo mbalimbali yanayowazunguka.



Amesema soko hilo limekuwa chafu kwa muda mrefu licha ya kuwa wawakilishi kutoka halmashauri ya jiji wamekuwa wakilisafisha lakini bado hali ya uchafu inaongezeka kutokana na wawakilishi hao kuwa wachache na  kukosa ushirikiano kutoka kwa wananchi
Kwa upande wa wanafunzi hao wamesema suala la kujitoa kufanya shughuli za kijamii kama kufanya usafi sehemu mbalimbali,kutembelea vituo vya watoto yatima hata wagonjwa,ni wajibu wa kila mtu na siyo wahusika pekee.
Wamesema lengo lao la kufanya hivyo ni kujenga na kudumisha uhusiano baina yao na jamii inayowazunguka kwani wao ni sehemu ya jamii na jamii ni wao hivyo ni jukumu lao kufanya hivyo.

UONGOZI WA SOKO LA MBAUDA UMEWASHUKURU WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI NA UTANGAZAJI KWA KUJITOLEA KUFANYA USAFI SOKONI HAPO.



Na ; Calorine Marwa.
Arusha
 
Wanafunzi wa madarasa ya Ruaha na Tarangire katika chuo cha uandishi wa habari na uatanagazaji Arusha wamefanya usafi katika soko la Mbauda ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao ya vitendo .

Baadhi ya wanafunzi hao wamesema kuwa wamefanya kazi hiyo kwa lengo la kujenga uhusiano mzuri na jamii pamoja na kutangaza jina la chuo na kijiweka katika nafasi nzuri 
Wanafunzi kutoka chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la mbauda jijini Arusha. (Picha na Calorine Marwa , ruaha media)
.Naye kwa upande wake Afisa wa afya wa kata ya Sombetini Bi. Betha Kitagoamewashukuru wanafunzi hao kwa kuwaunga mkono katika swala la usafi na kuahidi kuwaelimisha waliopo nyuma yao kwa kuendeleza usafi katika eneo hilo .

Bi . Gitago amesema kuwa wanakabiliwa na tatizo la wafagiaji wa soko hilokwani wapo watatu tu jambo ambalo linarudisha nyuma suala nzima la uasafi  katika soko hilo .

Aidha mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo Bw Hassan Athuman amesema amefurahishawa na zoezi hilo na kuwapongeza wanafunzi hao kwa kujitolea kufanya usafi n a kuwaomba waendeleena umoja huu ili kujenga uhusiano mzuri na jamii 

CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA {AJTC} CHAJIZOLEA SIFA KUTOKA UONGOZI WA SOKO LA MBAUDA.


Na ; Yusuph Mbata
Arusha
Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha{AJTC}, kimesifiwa na uongozi wa soko la Mbauda, kufuatia usafi uliofanywa na wanafunzi wa chuo hicho siku ya juma nne asubuhi.

Akitoa shukrani hizo wakati akizungumza na waandisi wa habari, afisa masoko wa kata ya Sombetini Bi. Beatha Gitagno. Amesema ni kitendo cha aina yake kilichofnywa na wanafunzi hao, na nivyema kuigwa na hata jamii nzima.

‘’Kwakweli tumefurahishwa sana kitendo hiki kilihofanywa na wanachuo hawa, sababu  ni wanafunzi wachache sana wanaweza kujitoa kufanya kazi za kijamii’’ alisema bi. Beatha
 
Wanafunzi kutoka chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la mbauda jijini Arusha (Picha na Yusuph Mbata , ruaha class)

Hata hivyo baadhi ya wafanya biashara katika soko hilo, wametoa wito pia kwa vyuo vingine kuiga kile kilichofanywa na wanafunzi hao. Kwakuwa itawajenga kiakili, kimwili hata kujenga ushirikiano na jamii.

Mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho,aliyejitambulisha kwa jina la Mbaraka Yahaya  amesema hiyo kwao ni moja ya masomo. Hivyo ni wajibu wao kufanya hivyo na nilazima wajifunze kwa nadharia na  vitendo pia.

‘’Sisi hii kwetu ni moja ya masomo, na ili kufikia malengo yetu. Ni lazma tujifunze kwa vitendo zaidi. Kuna somo linaitwa Public Relations ,kutoka kwenye kipengele cha PR campaign ambapo ilitulazimu kufanya kazi za kijamii.’’ Mbaraka alisema

Kwa upande wa Mkufunzi wa chuo hicho, ambae pia ni mwalimu wa somo hilo Madam Velediana. Alitoa shukrani zake kwa uongozi wa soko hilo, kwani walipokelewa kwa ukarimu tangu siku ya kwanza. Na kuonyeshwa ushirikiano wakutosha kutoka kwa viongozi hao.

Akipongeza chuo kwa usafi




Na Gilbert Massawe, Arusha

AFISA wa Afya katika kata ya Sombetini jijini Arusha, Beatha Gtaguo, amekipongeza chuo Cha  Uandishi  wa habari na Utangazaji Arusha, kufuatia  kujitolea kufanya Usafi katika soko la mbauda  kama mchango wao kwa jamii.

Akizungumza  na website ya chuo Beatha Gitaguo alisema kuwa wamefurahishwa na jambo hilo  kwani ni ushirikiano mzuri kati ya chuo na jamii inayowazunguka na kufanya hivyo ni kuwaelimisha  wananchi wengine kujitolea katika kazi za jamii.
 
Mwalimu wa chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Arusha, Verediana Akonay (kulia), na mwanafunzi wa chuo hicho Happiness Sarakikya, wakipeleka mfuko wa takataka katika soko la Mbauda jijini, Arusha jana. Picha na Gilbert Massawe
Hata hivyo, Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa  habari wamejitolea  kufanya usafi katika soko hilo kama mojawapo ya shughuli za kijamii ili kuonyesha mfano mzuri kwa jamii inayowazunguka.

 “Tumeshukuru kwa ujio wenu na kutuunga mkono katika swala la usafi na wanajamii wamejiuliza maswali kutokana na kile mlichokifanya eneo hili,” alisema   Beatha 


Alisema mojawapo mwa changamoto inayoikabili soko hilo ni Uhaba wa wafanyakazi wa kufagia, ambapo wapo wafanyakazi watatu wanaosafisha eneo hilo na miundo mbinu ya soko hilo haijakaa sawa hivyo huwapa wafagiaji tabu wakati wa ufagiaji.

UONGOZI WA SOKO LA MBAUDA UMEWASHUKURU WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI NA UTANGAZAJI KWA KUJITOLEA KUFANYA USAFI SOKONI HAPO.



Na ; Salma Juma , Ruaha Class.
Arusha

Wanafunzi wa madarasa ya Ruaha na Tarangire katika chuo cha uandishi wa habari na uatanagazaji Arusha wamefanya usafi katika soko la Mbauda ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao ya vitendo .

Baadhi ya wanafunzi hao wamesema kuwa wamefanya kazi hiyo kwa lengo la kujenga uhusiano mzuri na jamii pamoja na kutangaza jina la chuo na kijiweka katika nafasi nzuri 
Katika picha ni wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakifanya usafi katika soko la Mbauda kwa lengo la kutengeneza uhusiano mzuri na jamii (Picha na Salma Juma , ruaha class)