Wednesday, 28 January 2015

UMEIONA GAME YA CHELSEA NA LIVERPOOL








Andre Ayew aipeleka Ghana Robo fainali AFCON


CAIRO, Misri
MSHAMBULIAJI nyota  Andre Ayew aliipa Ushindi Muhimu Timu yake ya Ghana uliopa tikeki ya kucheza  Robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika katika kundi C, baada ya kuilaza South Afrika kwa mabao 2-1.

Vijana wa Kocha Avram Grant walikuwa wa kwanza kufunga Ubao wa mabao baada ya staika wake Mandla Masango kuweka kimiani bao la kwanza mnamo dakika ya 17, lililodumu kipindi cha kwanza.
Alikuwa  John Boye aliyebadilisha matokeo ndani ya dakika 17 baadae ushindi ulioupa Ghana nguvu ya kushambulia ngome ya Afrika Kusini.
Hata hivyo, Ayew alifunga ubao wa mabao kwenye dakika 83, na kuihakikishia Ghana kuingia raundi ya pili.
Ghana, ilimungiza nyota wake Wakaso Mubarak aliyechukua nafasi ya Emmanuel Agyemang-Badu, lakini bado ilikuwa moto wa kuotea mbali, ingawa wasiwasi ulienea kwa kutokosekana kwenye mchezo kwa nyota wa Afrika Kusini, Khuzwayo baada ya kusumbuliwa na  misuli nusu saa kabla ya mpira kuanza.

Wakati huo huo Senegali imejikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kupokea kipigo kilichovunja rekodi yao dhidi ya Algeria, kufuatia kuzabwa mabao 2-0. 
Senegal imesogea hadi nafasi ya tatu nyuma ya Algerians baada Ghana kuibuka na Ushindi dhidi ya Afrika Kusini.

Algeria ilikuwa bora katika dakika nane za kipindi cha pili baada ya staika Nabil Bentaleb kuzifumania nyavu za Senegal kabla ya
Riyad Mahrez kufunga bao la kwanza katika mchezo uliopigwa katika dimba la Mongomo.


Friday, 23 January 2015

habari : biashara ya nyama choma jijini Aruasha


Mfanyabiasha ra ya nyama choma akiandaa nyama kwa ajili ya wateja (Picha na Yusuph Mbata , ruaha media)

Wafanyabiashara wa nyama choma wakiendelea na uchomaji wa nyama katika baa zilizopo Morombo jijini arusha ( Picha na Alexabder Mgige , ruaha media )

Habari picha : wanawake wakisakata kabumbu


Timu ya wasichana ya wanafunzi wa level 5 kutoka katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha waliovaa jezi za bluu wakiwasalimia wachezaji wenzao wa level 4 kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki katika uwanja wa FFU (Picha na Hosiana Zakayo ,ruaha class)
Wachezaji wa timu ya level 4 katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo .(picha  na Emmannuel Masao , ruaha media)

Thursday, 22 January 2015

Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha AJTCwakiwa ndani ya studio yao ya redio wakifanya mazoezi ya vitendo

 Mmoja wa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari  na utangazaji akifanya mazoezi ya vitendo  ndani ya studio zao za redio zilizopo chuoni hapo:PICHA NA ANGELA RAPHAEL,Ruaha class

Angalia wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari (AJTC) wakiwa katika mafunzo ya somo la computer


HABARI PICHA WANAFUNZI WAKIJIFUNZA KWA VITENDO

Wanafunzi wanaosomea uzalishaji wa vipindi wakiwa katika studio za uzalishaji wa vipindi za chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wakiendelea na mazoezi aliyesimama mwenye shati la bluu ni mwalimu Elihuruma Chao ( picha na Calorine Marwa ;ruaha class)

Picha ya jengo la Utawala la chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Arusha (picha na Pendo Mbasee;ruaha class)

HABARI PICHA : Wanafunzi wa Ualimu wakiwa darasani

Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha wanaosomea ualimu wakiwa darasani wakijisomea (Picha na Salma Juma ;Ruaha class)
Mwalimu Elice akikagua kazi za wanafunzi wanaosomea ualimu katika chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Arusha (Picha na Zainabu Thabiti ; Ruaha class)

Wednesday, 21 January 2015

PICHA; MATUKIO YA WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA WAKATI WA MAZOEZI YA VITENDO

 HABARI NA, VICTOR SIMEO NA MUBARAKA.  RUAHA CLASS
Wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) Wakisikiliza kwa makini Vipindi vya Radio katika ukumbi wa chuo hicho. PICHA NA, VICTOR SIMEO
Baadhi ya wanafunzi Wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Wakisikiliza matangazo baada ya kumalizika kwa mazoezi ya vitendo katika ukumbi wa chuo hicho. PICHA NA, MUBARAKA YAHAYA

HABARI PICHA ZA MATUKIO YA MWAKA MPYA WA 2015 JIJINI ARUSHA

watoto wakisherehekea kuupokea mwaka mpya wa 2015 katika kanisa la KKT usharika wa ungalimited


burudani zikiendelea

Thursday, 15 January 2015

Kampuni za teknolojia zatoa mipango yao

Na Martin Massawe

Heather Watson atinga nusu fainali

Mcheza tennis namba moja wa Uingereza, Heather Watson, amefanikiwa kutinga nusu fainali.
Watson aliibuka kidedea kwa kumshinda Roberta Vinci katika michezo ya kimtaifa ya Hobart.
 

Mrembo wa dunia anasurika kifo kisha urembo

Mwanamke aliyemaliza katika nafasi ya pili ya mashindano ya urembo amedai kupenda sana kujiweka nakshi bandia nusura kumletee umauti.
Andressa Urach alimaliza wa pili katika mashindano ya urembo ambapo mashabiki walimpigia mwanamke waliyehisi kuwa na makalio mazuri zaidi katika nchi yao kupitia kwenye mtandao wa internet.
Ili kujiongeza urembo, Urach aliambia jarida la Daily Mail la Uingereza kwamba alidungwa sindano za kemikali ili kufanya makalio yake kuwa makubwa pamoja na kuongeza ukubwa wa miguu yake.
Lakini mnamo mwaka 2013, mwili wake ulianza kuoza ndani.
Athari za kujiweka urembo bandia zilianza kumwandama wakati Urachhadi madaktari wakalazimika kutoa kemikali hizo kutoka mwilini mwake mwezi Novemba kwa kuchimba mashimo katika mapaja yake.
Mwili wake ilipatwa na mshtuko kwa sababu ya ugonjwa alioupata kwa kutumia vifaa chafu vya matibabu mwilini mwake.

Daktari mmoja wa kurekebisha na kutibu athari zinazotokana na urembo bandia alisema ugonjwa aliopuata Urach ulitokana vifaa chafu.
Madaktari hata hivyo waliweza kuokoa maisha yake lakini hadi leo anatumia tu kiti cha magurudumu na miguu yake ina mashimo mwengi ambayo madaktari waliweza kutoboa ili kutoa kemikali zenye sumu alizotumia kuongeza ukubwa wa makalio na miguu.
''Ninalipia makosa yangu leo kwa sababu nilitaka urembo kwa kila hali, ili nionekane kuwa kamili. Mungu ananiadhibu'' Urach aliambia Mail.
''Lakini badala ya kujiongeza urembo, niliharibu mwili wangu na sasa hata hauna sura.''

Wednesday, 14 January 2015

Dk. Slaa aeleza alivyomnasa anayedaiwa kujiita Jaji Samatta

Na SUZANE CHEDDY

15th January 2015
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Hai kwamba, kabla ya kuchukua hatua ya kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk. Edward Hosea, akimuomba ofisi yake ifanye uchunguzi wa kina kumbaini mtu anayejiita Jaji Barnabas Samatta, alimpa mkewe achunguze jina la mtu huyo.

Maalim Seif: Ukawa tishio kwa CCM

15th January 2015
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema matokeo ya uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwezi uliopita ni somo kwa vyama vya upinzani kuwa vitakaposhikamana hakuna nguvu ya Polisi wala Jeshi itakayowazuia wasikamate dola.

Dk. Slaa aeleza alivyomnasa anayedaiwa kujiita Jaji Samatta

15th January 2015
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Hai kwamba, kabla ya kuchukua hatua ya kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk. Edward Hosea, akimuomba ofisi yake ifanye uchunguzi wa kina kumbaini mtu anayejiita Jaji Barnabas Samatta, alimpa mkewe achunguze jina la mtu huyo.

Alidai kwamba aliamini mkewe, Josephine Mushumbuzi, angeweza kumtambua kwa haraka mtumiaji wa simu namba (0754 013237) anayejiita Jaji Samatta kwa kuwa mkewe ni mtaalam mbobezi wa Teknolojia ya Mawasiliano ya Kompyuta na aliweza kumjua mtu huyo baada ya kumtumia mhamala wa Sh. 500 kwa njia ya M-Pesa

Maofisa wa serikali kortini mgawo Tegeta Escrow

15th January 2015
Mkurugenzi wa Huduma ya Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma (kulia) na picha ya kushoto, Mhandisi wa Mamlaka ya Umeme Vijijini (Rea),Theophillo Bwakea, wakifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana kujibu mashtaka ya rushwa baada ya kudaiwa kupokea mgao wa fedha zinazohusiana na akaunti ya Tegeta Escrow. P
 
Maofisa wawili wa serikali,  Rugonzibwa Mujunangoma na Theophillo Bwakea,  wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashitaka ya rushwa baada ya kudaiwa kupokea mgao wa Sh. Milioni 485.1 kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)  walizohamishiwa na James Rugemalira.

Raundi ya pili taifa Cup wanawake Jumamos

Na.Happy Ernest,ruaha class

Kikosi cha timu ya Taifa
Mechi za kwanza za raundi ya pili ya mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake-Tanzania (Taifa Cup Wanawake) zinachezwa wikiendi hii (Januari 17 mwaka huu) kwenye miji minane tofauti nchini.
Timu tisa zilizofuzu kutoka raundi ya kwanza baada ya mechi za nyumbani na ugenini akiwemo mshindwa (best loser) zitaungana na Ilala, Kinondoni na Temeke kucheza raundi ya pili. Mechi za marudiano za raundi hiyo zitachezwa Januari 21 mwaka huu.
Hatua ya robo fainali itakayochezwa Januari 26 na 27 mwaka huu pamoja na nusu fainali na fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Proin Promotions itafanyikia jijini Dar es Salaam.

Paula Radcliffe kustaafu riadha

Na.Angel Raphael,ruaha class

o

Paula Radcliffe

Mwanariadha Paula Radcliffe raia wa Uingereza anatarajia kustaafu kucheza mchezo huo mwishoni mwa mwezi wanne.
Paula mwenye umri wa miaka 41, ambaye alishinda mara tatu katika michuano ya marathoni ya
Radcliffe, ambae aliweka rekodi ya kukimbi kwa masaa mawili dakika 15 na sekunde 25 katika michuano ya mwaka 2003
Mratibu wa riadha wa London Hugh Brasher. “Amesema tumemteua Paula kushiriki michezo ya marathoni kwa mara mwisho kabla hajapumzika”.
Mbio hizo za marathoni zitafanyika tarehe 26 mwezi wa nne.